Karibu ABlinkA
Home of innovations
Rejea Edeni
Nyumba ya Ubunifu, Afya na Ustawi
ulimwenguni kuna nini?
KUHUSU SISI
Dhamira yetu ni kuhamasisha, kuratibu, kufundisha na kusaidia vijana na wanawake katika jamii kutumia fursa zilizopo kubuni bidhaa na huduma zenye ubora wa juu, zinazotatua changamoto za kijamii, kutengeneza ajira, na kuinua vipato kwa kujiajiri na kuajiri wengine.
KUHUSU SISI
Dhamira yetu ni kuhamasisha, kuratibu, kufundisha na kusaidia vijana na wanawake katika jamii kutumia fursa zilizopo kubuni bidhaa na huduma zenye ubora wa juu, zinazotatua changamoto za kijamii, kutengeneza ajira, na kuinua vipato kwa kujiajiri na kuajiri wengine.
Miradi
Ufugaji wa Kuku na Samaki
Tunatoa mafunzo kuhusu ufugaji wa kuku na samaki kwa njia za kisasa zinazohakikisha uzalishaji bora na faida kubwa. Wageni wanajifunza kuhusu uchaguzi wa mbegu bora, ulishaji, udhibiti wa magonjwa, na mbinu...
Kilimo cha Matunda na Mboga
Tunalenga kuzalisha matunda na mboga zenye thamani kubwa sokoni, hasa mijini kama Morogoro. Wanaoshiriki wanajifunza kuhusu uchaguzi wa mazao, matumizi ya mbolea asilia, umwagiliaji...
Usindikaji wa Bidhaa na Elimu kwa Jamii
Tunatoa mafunzo ya usindikaji wa mazao ili kuongeza thamani na kupanua soko. Hii inahusisha usindikaji wa bidhaa za shamba, kutengeneza bidhaa za afya ya ngozi kama sabuni na mafuta ya asili...
Huduma Zetu
Karibu ABLINKA, mahali ambapo huduma zinakutana na ubora wa hali ya juu ili kukupa uzoefu wa kipekee. Tunajivunia kukuletea huduma mbalimbali zinazokidhi mahitaji yako kwa viwango vya juu, mazingira tulivu, na huduma za kibinafsi.
Malazi
Tunatoa malazi ya kifahari kupitia mfumo wa Bed & Breakfast (B&B). Vyumba vyetu ni safi, vya kisasa, na vinakupa utulivu wa hali ya juu.
Ubunifu
Furahia vyakula vya asili vilivyoandaliwa kwa viwango bora, pamoja na matunda freshi kutoka shambani. Pia, tunatoa vinywaji vya asili kwa afya bora
Kumbi
Tunakodisha kumbi ndogo na za kati kwa mikutano, semina, na sherehe. Mazingira yetu ni tulivu na yanafaa kwa kila tukio lako maalum
Afya na Mazoezi
Tunatoa mazoezi, massage, na tiba asilia kwa afya njema. Programu zetu zinakuwezesha kujenga mwili wenye nguvu na kupunguza msongo wa mawazo
CEO
Dkt. Bunini Manyilizu ni Daktari wa Tiba ya Binadamu aliyehitimu Chuo Kikuu cha Muhimbili, mwenye Shahada ya Uzamili katika Afya ya Jamii na Shahada ya Uzamivu katika Usalama wa Afya dhidi ya Sumu. Ni mkufunzi, mtafiti na mwandishi anayejulikana kwa uwezo wake wa kufafanua masuala ya kisayansi kwa lugha rahisi. Akiwa mshauri aliyethibitishwa na SIDO, amejikita katika kuwawezesha wajasiriamali kupitia usindikaji wa bidhaa za lishe, urembo na utanashati.
Pia anahudumu katika Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambako anashughulika na Tafiti, Ubunifu na Maendeleo ya Kisayansi. Ana mtandao mpana wa wanasayansi, watafiti na wabunifu ndani na nje ya Tanzania. Dkt. Bunini ni Mwanzilishi wa ABlinkA Trust iliyoko Morogoro, inayolenga kuhamasisha jamii katika kujitegemea, kuboresha maarifa ya Afya-Kinga, Kilimo, Ufugaji, Usindikaji wa bidhaa, na matumizi ya Teknolojia na Ubunifu kwa ustawi wa jamii.
Business
Startup, Management, Marketing, and Sales
Research
Concept proposal, Data Entry, Report Editing Services
Book writing and publication
Teaching and learning methods are applied) accordingly
Creativity and Innovativeness
Concepts of innovation and innovation, Exposure and practical
Tunaweza kukuunganisha kila mahali
Tunakuunganisha na wataalamu, taasisi, teknolojia nafuu, ubunifu na fursa ili kukusaidia kufikia malengo yako ya ujasiriamali na ajira.
