Sisi ni Nani?
Dhamira Yetu
Dhamira yetu ni kuwahamasisha watu wakubali utamaduni wa ubunifu katika kila wanachofanya. Tunaamini katika kulenga mbali na kuwa na maono makubwa, kushinda vikwazo, kukumbatia ubunifu, na kubadili mawazo mazuri kuwa bidhaa au huduma ili kuleta mabadiliko maishani. Kupitia kituo chetu cha ubunifu, tunalenga kuwahamasisha, kushirikiana, na kuwawezesha watu binafsi, kuwaunganisha watu na mahali ambapo wanaweza kupata msaada, kwa mafanikio na ukuaji endelevu katika maendeleo yao. Tumejitolea kuwasaidia kugundua fursa, kuongeza thamani katika kila hatua, na kukuza mabadiliko yenye maana kupitia ubunifu.
Maono Yetu
Kuwa timu ya ubunifu na wajasiriamali waliojaa baraka na furaha, wanaoishi kwa mafanikio, ili kuwa wajasiriamali na wabunifu wa mvuto kwa jamii.
