MIRADI
Miradi ya ABLINKA
Kubadilisha Maisha Kupitia Ubunifu na Uzalishaji
ABLINKA ni jukwaa bunifu linaloleta mageuzi katika kilimo, ufugaji, na usindikaji wa bidhaa kwa kuongeza thamani na kuboresha maisha. Tunatoa fursa za kujifunza, kuwekeza, na kupata kipato endelevu, tukihamasisha teknolojia na mbinu za kisasa kuboresha uzalishaji na masoko.
Mradi
Ufugaji wa Kuku na Samaki
Tunatoa mafunzo kuhusu ufugaji wa kuku na samaki kwa njia za kisasa zinazohakikisha uzalishaji bora na faida kubwa. Wageni wanajifunza kuhusu uchaguzi wa mbegu bora, ulishaji, udhibiti wa magonjwa, na mbinu bora za soko. Pia, tunahamasisha matumizi ya mifumo ya ufugaji wa kisasa kama ufugaji wa samaki katika vizimba na utunzaji wa kuku kwa njia rafiki kwa mazingira ili kuongeza tija na ubora wa bidhaa.




Mradi
Kilimo cha Matunda na Mboga
Tunalenga kuzalisha matunda na mboga zenye thamani kubwa sokoni, hasa mijini kama Morogoro. Wanaoshiriki wanajifunza kuhusu uchaguzi wa mazao, matumizi ya mbolea asilia, umwagiliaji, na udhibiti wa wadudu kwa njia rafiki kwa mazingira. Mbali na uzalishaji, tunatoa mafunzo ya jinsi ya kuhifadhi na kufungasha mazao ili kuhakikisha ubora wake unadumu kwa muda mrefu na kuvutia soko la kitaifa na kimataifa.



Mradi
Bustani ya Miti Dawa
ABLINKA imeanzisha bustani ya miti dawa, ambapo wanajamii watajifunza kuhusu mimea dawa ya asili kwa ajili ya tiba na afya kinga. Bustani hii inaweza kutumika katika kuthibiti magonjwa mbalimbali. Lakini pia, watafiti wa dawa wanaweza kupata fursa ya kujifunza, na kufanya utafiti zaidi kwa mimea dawa iliyoko bustanini. Mimea dawa hii itakuwa na taarifa za tafiti ambazo zimekwisha kufanyika tayari na mimea dawa ambayo tayari inatumika katika makabila kadhaa hapa Tanzania.



Mradi
Usindikaji wa Bidhaa na Elimu kwa Jamii
Tunatoa mafunzo ya usindikaji wa mazao ili kuongeza thamani na kupanua soko. Hii inahusisha usindikaji wa bidhaa za shamba, kutengeneza bidhaa za afya ya ngozi kama sabuni na mafuta ya asili, na elimu kwa jamii kuhusu kuongeza thamani ya mazao. Washiriki wanajifunza kuhifadhi bidhaa, viwango vya ubora, na ufungashaji bora wa kisasa. Kupitia programu hizi, wanajamii wanapata ujuzi wa kujiajiri, kuongeza kipato, na kuboresha ustawi wa familia zao kwa njia endelevu.



ABLINKA inalenga kuinua maisha ya wanajamii kwa maarifa na fursa za kuboresha uzalishaji. Tunakaribisha wadau kushirikiana nasi kuleta maendeleo endelevu katika kilimo, ufugaji, na usindikaji.
Ajira mindset
PRACTICAL DEMONSTRATION UNITS
Kama nyumba ya ubunifu ina vitengo mbalimbali vya huduma, sisi ndio kichocheo cha safari yako ya ubunifu. Mazingira yetu yameandaliwa kuwezesha wajasiriamali na wanaojipanga kuwa wabunifu.
Tuna:
- Fundisha, onesha na fanya kwa vitendo hatua kwa hatua katika mapishi na lishe, usindikaji, vyakula na bidhaa za ngozi n.k kulingana na mapenzi yako.
- Wataalam kutoka ndani na nje ya makao yetu watakaokuelekeza, kutoka kwa ubunifu hadi kwenye utengenezaji wa pesa katika mazingira ya kisasa.
- Kuunganisha na rasilimali kama upatikanaji wa teknolojia rahisi na ya bei nafuu, na ushauri wa kitaalamu.
- Kuunganisha na watu wazoefu kwenye tasnia, waliofanikiwa na washirika, na viongozi wa sekta husika ili kupanua mtandao wako na fursa zako.
- Kushirikisha katika maonesho ya wajasiriamali, teknolojia, na ubunifu kupitia maonesho.
Mustakabali wako wa ubunifu unaanzia hapa!
